Madhara ya Ukatili wa kijinsia

 


Madhara ya haraka ni kama maumivu, michubuko, kuvunjika mifupa, kuvuja damu na hata kupelekea kifo. Huweza kuleta madhara ya muda mrefu kimwili na kijamii.

  Huweza kuleta tabia hatarishi, kuvuta sigara, matumizi ya pombe na dawa za kulevya. Kuathirika katika ukuaji wa mtoto kiakili na maendeleo ya chini kitaaluma. Huweza kusababisha magonjwa ya ngono na maamumbiizi ya Virusi vya Ukimwi. Kujiingiza katika ngono hatarishi hasa kwa kukosa kujiamini au kujiona hana thamani. Athari za kijamii ni kama gharama za uchunguzi, kushughulikia mashitaka ya ukatili kwa wanawake na kutekelezwa kwa Watoto na tabia za ulevi au uhalifu ukubwani

Comments