Wazee ni moja ya kundi lenye mahitaji maalum kilishe kutokana na mabadiliko mengi ya kimwili hivyo kuwa katika hatari kubwa ya kupata utapiamlo. Wazee wanashauriwa kula mlo ulio na virutubisho kamili ili kuupa mwili nguvu ya kutosha. Wazee wanashauriwa kupunguza vyakula vya mafuta, sukari, chumvi pamoja na kuongeza ulaji wa matunda na mbogamboga kwa wingi katika kila mlo. Wazee wanashauriwa kushughulisha mwili kulingana na hali zao za kiafya na umri mfano; kutembea, kuendesha baiskeli au kufanya kazi ndogo ndogo. Wazee wanashauriwa kupima afya zao angalau mara 2 kwa mwaka ili kupata ushauri wa vyakula na namna ya kujikinga na magonjwa mbalimbali, lakini pia kupata matibabu stahiki pale yanapohitajik
Comments
Post a Comment