Huduma ya kwanza ni msaada wa haraka anaopewa mtu aliepata ajali au kuugua kabla ya kumpeleka kituo cha huduma za afya ili kuokoa maisha na kupunguza madhara.
Kabla ya kutoa huduma ya kwanza tambua aina ya dharula, hakiki usalama wa mazingira, majeruhi na mtoa huduma ya kwanza.
Baadhi ya dharula zinazohitaji huduma ya kwanza ni ajali, kuvuja damu, moto, kuzama majini, kuanguka, kupoteza fahamu, kuumwa nyoka, mbwa, fisi, nge, nyuki.
Kwa taarifa, Msaada au Ushauri Piga Simu zifuatazo bure: WIZARA YA AFYA - 199, ZIMAMOTO - 114, POLISI - 112, TAKUKURU - 113, Huduma ya simu kwa mtoto - 116
Comments
Post a Comment