Trakoma/Vikope

 


Trakoma au Vikope ni ugonjwa unaosabishwa na bakteria Klamidia trakomati. Maambukizi husababisha kukwaruza kwa sehemu ya ndani ya vigubiko vya macho. Mkwaruzo huu unaweza kusababisha maumivu ya macho, kuharibika kwa sehemu ya nje ya macho au konea, na hatimaye upofu. Bakteria anayesababisha ugonjwa husambazwa kwa mgusano wa macho au mapua wa moja kwa moja au usiokuwa wa moja kwa moja na mtu aliyeambukizwa. Mgusano wa macho au mapua usiokuwa wa moja kwa moja unajumuisha kupitia nguo au nzi waliogusa mtu aliyeambukizwa. Watoto husambaza ugonjwa mara yingi zaidi ya watu wazima. Mazingira chafu, maeneo yaliyo na watu wengi, na mahali pasipo na maji safi ya kutosha na choo yanachangia usambazaji wa gonjwa hili. Dalili zinaweza kua macho kuwasha, kuwa na maumivu, kuvimba, kutoa uchafu, machozi na kutopenda mwanga .Vilevile homa, maumivu ya mitoki (tezi)na mwili kuchoka. Unaweza kuepuka ugonjwa huu kwa kuzuia maambukizi, kupata matibabu mapema uonapo dalili, pia kuweka mazingira safi ili kuzuia nzi na usafi wa uso kwa maji safi. Upasuaji huweza kuhitajika kulingana na hatua ya ugonjwa. Dawa za matibabu hupatikana kwa urahisi katika vituo vya afya, tiba ya mapema ni muhimu kuepusha upofu.

Comments